Mkufunzi wa makipa wa Yanga, Razack Siwa amesema katika mechi zilizobaki mashabiki watarajie kumuona mlinda lango Ramadhani Kabwili akiwa langoni
Siwa ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui Fc utakaopigwa kesho Jumapili uwanja wa Benjamin Mkapa
Siwa alikuwa akijibu swali la mwanahabari aliyehoji kwa nini Kabwili hapewi nafasi?
"Mabadiliko ni sehemu ya mchezo na kila mechi inakuwa na mpango wake. Hivyo naweza sema mnaweza kumuona kabwili akiwa langoni kwenye baadhi ya mechi pia na mabadiliko mengine ambayo tunaweza kufanya kulingana na mahitaji ya mchezo," alisema Siwa
Jana uongozi wa Yanga ulitangaza kumsimamisha mlinda lango Metacha Mnata kufuatia tukio la kuwatukana mashabiki baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-2 juzi
Metacha aliomba radhi lakini hatma yake inasubiri kikao cha Kamati ya Nidhamu
Sasa Yanga imebakiwa na walinda lango wawili, Farouk Shikhalo na Kabwili