Uongozi wa klabu ya Yanga unaendelea kupokea maoni ya wapenzi, wanachama na mashabiki wake kuelekea Mkutano Mkuu utakaofanyika Juni 27 mwaka huu
Baraza la Wazee wakiongozwa na Mzee Mangoma jana walifanya Mkutano na Wanahabari ambapo walitoa maoni yao wakipinga baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba iliyopendekezwa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema sasa ni kipindi cha kukusanya maoni hivyo wazee nao wametimiza wajibu wao
"Kuelekea Mkutano Mkuu tunawasihi Wanachama wa Yanga waendelee kuwasilisha maoni yao. Tumepokea maoni ya Wazee wetu, tunawashukuru sana kwa maoni yao. Wanachama muendelee kuwasilisha maoni yenu"
"Tulichonacho sasa ni rasimu ya Katiba ambayo inahitaji maoni na mapendekezo ya Wanachama ili kuboreshwa kabla ya kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura," alisema Bumbuli
Zimebaki takribani siku 12 kufanyika Mkutano Mkuu wa Wananchama. Zoezi la kukusanya maoni ya Wanachama litafungwa Juni 20