Baada ya usajili wa Shabani Djuma kutoka klabu ya AS Vita, Yanga inatajwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa Mcongomani mwingine Mercey Vumbi Ngimbi anayechezea klabu ya Meniema United
Ngimbi ni kiungo akiwa na msimu mzuri kwenye ligi kuu ya DR Congo iliyomalizika hivi karibuni akifunga mabao saba na kutoa pasi tisa za mabao
Ameisaidia Meniema kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya TP Mazembe iliyomaliza katika nafasi ya pili huku AS Vita wakiibuka mabingwa
Kama Yanga itafanikisha usajili wake, atakuwa Mcongomani wa nne kusajiliwa na Yanga baada ya Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe na Shabani Djuma
Aidha atakuwa mchezaji wa pili kusajili kutoka klabu ya Meniema baada ya Kisinda ambaye alitua Yanga akitokea klabu hiyo iliyokuwa imemtoa kwa mkopo AS Vita
Kwa sasa nyota wengi huko DR Congo wanatamani kuja nchini kucheza Yanga kutokana na mahusiano mazuri ambayo Yanga wametengeneza na klabu za Congo
Aidha utaratibu wa usajili ambao GSM wanautumia kwa kwenda kumalizana na wachezaji katika klabu zao, unawapa uhakika kuwa wanasajiliwa na timu ambayo haina mambo ya ujanja ujanja