Kiungo fundi wa Yanga Haruna Niyonzima 'Baba Mzazi' alikosekana kikosini kwa wiki kadhaa kutokana na matatizo ya kifamilia
Habari njema ni kuwa Niyonzima amemaliza changamoto zilizokuwa zikimkabili na sasa amerejea kuwatumikia Wananchi
Kulikuwa na tetesi kuwa nyota huyo aliomba mkataba wake uvunjwe, yeye mwenyewe alikanusha na kusisitiza bado ni mchezaji wa Yanga akiendelea kutumikia mkataba wake aliosaini mwezi Disemba 2020
Niyonzima hakuwa na wakati mzuri wakati wa kocha Cedric Kaze, bado hajatumika na kocha Nasreddine Nabi kutokana na changamoto zilizokuwa zikimkabili
ADVERTISE HERE