Jumapili Juni 06 saa moja jioni mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili African Lyon ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Ni moja ya michezo ambayo kocha Nasreddine Nabi aliihitaji ili kuwapima wachezaji wake kuelekea ngwe ya lala salama ligi kuu ya Vodacom pamoja na mchezo wa nusu fainali kombe la FA
Wananchi wameaswa kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kuwashuhudia nyota wao kina Tuisila Kisinda, Abdallah Shaibu, Makapu, Farid Mussa, Zawadi Mauya, Kibwana, Adeyum, Farouk, Kabwili na wengine kibao...!
Mchezo huo utatoa nafasi kwa wachezaji ambao hawana majukumu ya timu za Taifa kuwaburudisha mashabiki wao
Nyota sita wanaokabiliwa na majukumu ya timu za Taifa ni Metacha Mnata, Dickson Job, Bakari Nondo, Feisal Salum, Mukoko Tonombe na Yacouba Songne
Viingilio vya mchezo huo VIP ni Tsh 5,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-