Mchezo wa kisasi dhidi ya Mbao FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2017
Mchezo wa kisasi dhidi ya Mbao FC
Siku ya mwisho ya mwaka 2017, Jumapili ya Disemba 31 Yanga itashuka kwenye dimba la CCM Kirumba kuikabili timu isiyotabirika, Mbao FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na upinzani uliojengeka msimu uliopita baina ya timu hizo.

Mbao FC ambayo iko kwenye msimu wake wa pili tangu ipande daraja, imekuwa haifungiki kirahisi inapocheza kwenye dimba lake la nyumbani.

Msimu uliopita imekutana na Yanga mara mbili katika dimba la CCM Kirumba na kuibuka na ushindi katika michezo yote.

Mchezo wa kwanza ulikuwa wa nusu fainali kombe la FA na Mbao FC kuindosha Yanga kwenye michuano hiyo kwa kuichapa bao 1-0.

Zikakutana tena kwenye mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu na kwa mara nyingine Mbao FC ikaibuka na ushindi wa bao 1-0.

Matokeo yaliyoipa Simba jeuri ya kwenda FIFA kudai alama tatu ili wachukue ubingwa baada ya kufungana na Yanga kwa alama 68 huku Yanga ikiwa imefunga mabao mengi zaidi.

Hata hivyo benchi la ufundi la Yanga lililo chini ya makocha wasaidizi Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa limeapa kufuta uteja dhidi ya timu hiyo.

Yanga iko chini ya makocha hao kufuatia kocha Mkuu George Lwandamina kufiwa na mtoto wake wa kiume.

Katika mchezo huo Yanga itamkosa mshambuliaji wake fundi wa mpira Ibrahim Ajib anayetumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kufikisha kadi tatu za njano.

Hata hivyo kurejea kwa mshambuliaji Amissi Tambwe kunatoa ahueni kwa Yanga kwani huenda akapangwa sambamba na Obrey Chirwa, kinara wa upachika mabao katika kikosi cha Yanga.

Licha ya kuanza mazoezi mepesi Thabani Kamusoko na Kelvin Yondani huenda wasiwe tayari kwa mchezo huo huku Donald Ngoma naye akitarajiwa kukosekana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’