Hatimaye Manji amerejea Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jun 2021
Hatimaye Manji amerejea Tanzania

Baada ya tetesi za muda mrefu, Mwenyekiti wa zamani klabu ya Yanga Yusufu Manji ni kweli amerejea nchini

Manji alijiuzulu Uwenyekiti wa Yanga May 23 2017 kutokana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kukabiliwa na kesi mbalimbali Mahakamani

Baada ya kutua hapo jana, alizuiliwa kwa muda na maofisa Uhamiaji kwa ajili ya kujiridhisha na masuala kadhaa na baadae aliruhusiwa

Tangu alipoondoka nchini, Manji alikuwa akiishi Marekani

Mkurugenzi huyo wa Makampuni ya Quality Group ni kama ameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alifungua milango kwa Wawekezaji waliokuwa wameondoka nchini kutokana na changamoto za hapa na pale, warejee kuendelea na shughuli zao huku Serikali ikiahidi kushirikiana nao katika kutatua changamoto hizo

Wiki iliyopita Mfanyabiashara, tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia kwa nyakati tofauti alihusishwa kutaka kuwekeza Yanga, nae aliwasili nchini na kufanya mazungumzo na Rais Samia ambapo aliwataka Wafanyabiashara na wawekezaji waliokuwa wameondoka kurejea nchini ili washirikiane na Serikali

Kurejea kwa Manji ni habari njema kwa Wananchi kwani upo uwezekano mkubwa pale mchakato wa Mabadiliko utakapokuwa umekamilika, anaweza kujitosa kununua hisa ili kuwa mmoja wa Wawekezaji ndani ya klabu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’