Baada ya mapumziko ya siku kadhaa, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini kujiandaa na mechi zinazofuta, ligi kuu ya Vodacom na kombe la FA

Wachezaji sita walioitwa timu za Taifa wameruhusiwa kwenda kujiunga na wenzao huku wachezaji wengine wakiendelea na program za mazoezi chini ya kocha Nasreddine Nabi
Juni 17 Yanga itacheza na Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Mwadui Fc na utapigwa Juni 20 hapo hapo kwa Mkapa
Baada ya mchezo huo Wananchi watahamishia nguvu zao kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Biashara United utakaopigwa kati ya Juni 24-27 mkoani Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi
ADVERTISE HERE