Kamati ya usajili Yanga wanalo la kujifunza

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
31 May 2021
Kamati ya usajili Yanga wanalo la kujifunza

Yanga leo imethibitisha kuachana na kiungo Carloh Carlinhos ambaye ameomba kuvunja mkataba wake kutokana na sababu za kifamilia

Carlinhos ameitumikia Yanga michezo isiyozidi 10 kwani muda mwingi amekaa nje akiuguza majeraha

Ni mmoja wa wachezaji ambao walitua Yanga na kuibua shamrashamra kubwa kwa mashabiki, kuondoka kwake mapema ni somo kwa Injinia Hersi Said na kamati ya usajili Yanga

Changamoto ya lugha na aina ya soka la Tanzania vimechangia yeye kuondoka mapema

Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini amekuwa na wakati mgumu kwendana na mazingira ya soka letu

Ndio maana muda mwingi aliutumia akiuguza majeraha kwani haikuwa rahisi kwake kucheza mechi ngumu hasa zilizopigwa nje ya jiji la Dar es salaam

Mchezo wake wa mwisho ulikuwa wa FA dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa Sumbawanga na Yanga kushinda bao 1-0

Carlinhos alipata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa takribani wiki tatu

Pengine ni wakati kamati ya usajili kuwatumia wakongwe waliopita zamani Yanga kufanya scouting ya wachezaji wanaotaka kusajiliwa

Usajili haupaswi kuwa uamuzi wa mtu mmoja, kila mdau atoe mapendekezo, iwepo timu ya kujiridhisha na waliopendekezwa kabla ya kusajiliwa

Sunday Manara, mmoja wa wakongwe walioacha alama kubwa Yanga, aliwahi kulalamika kuwa wachezaji wengi waliosajliwa wana uwezo wa kawaida

Wakongwe hawa wanaweza kuisaidia Yanga kusajili wachezaji ambao wataweza kumudu soka la Tanzania na pia kuisaidi timu

Unaweza kusema usajili wa Carlinhos umesababisha hasara kwani Yanga imetumia muda mwingi kumtibia kuliko muda ambao yeye alitumika uwanjani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’