Tunaanza hatua ya pili kuelekea Yanga Mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 May 2021
Tunaanza hatua ya pili kuelekea Yanga Mpya

Leo Wenyeviti na Makatibu wa Matawi ya klabu ya Yanga nchi nzima, watakuwa Makao Makuu ya klabu hiyo Jangwani kushiriki Semina ya Mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji

Juni 27 Yanga itafanya Mkutano Mkuu wa Mwaka, miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kujiri katika Mkutano huo ni Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu

Huu ni Wakati kwa viongozi wa Matawi kupatiwa elimu ya muundo na mfumo wa uendeshaji ambao Yanga itaanza kuutumia baada ya michakato yote kukamilika

Baada ya kupatiwa Elimu, viongozi wa Matawi watakuwa na jukumu la kuwasilisha Elimu hiyo kwa Wanachama wa Yanga katika Matawi yao ili kuhakikisha Juni 27 wanafanya maamuzi sahihi

Kwa ufupi, kulingana na rasimu ya Mabadiliko iliyowasilishwa hivi karibuni kwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla baada ya mchakato wake kukamilika, Yanga imekusudia kubadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka umiliki wa Wanachama kwa asilimia 100 na kuwa mfumo wenye mchanganyiko ambapo Wanachama watabaki na hisa asilimia 51 wakati hisa nyingine asilimia 49 zitauzwa kwa wawekezaji

Pia kutakuwa na Mabadiliko ya uongozi ambayo yatahitaji Katiba kufanyiwa marekebisho

Mfano, mfumo mpya utahitaji kuwa na Rais badala ya Mwenyekiti, Mtendaji Mkuu (CEO) badala ya Katibu Mkuu n.k

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’