Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mwadui Fc kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Ntibazonkiza alipata majeraha katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania mkoani Dodoma
Pamoja na kusafiri na timu mkoani Shinyanga, uongozi wa Yanga ulilazimika kumrejesha jijini Dar es salaam jana ili akapatiwe matibabu ya haraka
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbulia amesema Ntibazonkiza ameonana na daktari leo kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo kubaini ukubwa wa majeraha aliyopata
Nyota huyo amekuwa akikabiliwa na changamoto ya majeraha ya mara kwa mara
ADVERTISE HERE