Carlinhos, Yassin wakaribia kurejea kikosini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 May 2021
Carlinhos, Yassin wakaribia kurejea kikosini

Wachezaji Carlinhos na Yassin Mustafa wanatarajiwa kufanyiwa vipimo siku ya Jumatatu kubaini kama wamepona majeraha yaliyowaweka nje kwa wiki kadhaa

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli nyota hao walipaswa kukaa nje kwa wiki mbili kulingana na taarifa za majeraha yao

Aidha Bumbuli amesema beki Abdallah Shaibu 'Ninja' yeye ataendelea kukosekana kwa wiki moja zaidi

"Yassin na Carlinhos watafanyiwa vipimo na madaktari Jumatatu ili kuona kama wamepona sawasawa ili warejee kikosini. Wote walipaswa kukaa nje wiki mbili, muda ambao tayari umekamilika," alisema Bumbuli

"Ninja yeye bado anaendelea na kukosekana kwa wiki nyingine moja. Tunatarajia atakuwa tayari kurejea baada ya muda huo"

Habari njema pia ni kupona kwa kiungo Mapinduzi Balama ambaye sasa anatarajiwa kuanza mazoezi baada ya kufanyiwa vipimo juzi na kubaini amepona

Hata hivyo nyota huyo aliyekaa nje kwa takribani mwaka mmoja, hatarejeshwa kikosini moja kwa moja bali ataendelea na program maalum ya mazoezi kabla ya kujumuishwa na wachezaji wengine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’