Mwadui Fc ya kwanza kushuka daraja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 May 2021
Mwadui Fc ya kwanza kushuka daraja

Baada ya kushiriki Ligi Kuu kwa misimu sita mfululizo, Mwadui FC ya Shinyanga leo imeshuka rasmi daraja baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Prisons katika mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Mwadui Complex

Bao la mshambuliaji Mohamed Mkopi katika dakika ya 82, lilitosha kuifanya Prisons kupata ushindi huo ambao umeiwezesha kufikisha pointi 40 zilizowasogeza hadi nafasi ya saba katika msimamo wa ligi na kuwashusha rasmi Mwadui waliopanda daraja mwaka 2015.

Kipigo hicho kimeifanya Mwadui FC ibakie na pointi zake 19 huku ikibakiza mechi nne kabla ya kumaliza msimu, ambazo hata ikishinda zote, itamaliza ikiwa na pointi 31 ambazo haziwezi kuisaidia kutoka katika kundi la timu nne za mwisho zitakazoshuka daraja.

Kati ya mechi nne ambazo Mwadui FC imebakiza, moja itacheza uwanja wa nyumbani na baada ya hapo itakuwa na mechi tatu za ugenini

Wiki ijayo Mwadui Fc itacheza na Yanga mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam

Pia mwezi ujao watasafiri jijini Dar es salaam kuikabili Yanga kwenye mchezo wa duru ya pili ligi kuu ya Vodacom

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’