Siwa amtetea Shikhalo goli la Dube

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2021
Siwa amtetea Shikhalo goli la Dube

Mkufunzi wa magolikipa Yanga, Razak Siwa, amemtetea golikipa wake, Faroukh Shikalo kuwa bao alilofungwa katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam Fc halitokani na uzembe bali ni uwezo binafsi na ujuzi wa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube

Siwa amebainisha kuwa hawezi kumtupia lawama Shikalo kwa sababu mfungaji alitumia ufundi na ujuzi mkubwa wa kupiga mpira wa mbali na kuipa timu yake ushindi.

"Mpigaji alitumia ujuzi na alitumia akili ya kufunga, kufungwa haikuwa uzembe wa kipa wetu kwa sababu hata sisi tuliweza kupata nafasi waliyopata Azam FC kwa kupiga shuti la mbali na kushindwa kutumia vizuri nafasi,".

"Tulitengeneza nafasi nyingi hatukuweza kutumia kwa sababu hatukuwa watulivu ila wenzetu walipata walikuwa makini na utulivu mkubwa wa kupata ushindi huo," alisema Siwa.

Aliongeza baada ya matokeo mabaya waliyopata juzi, wanaenda kufanyia kazi upungufu wote uliojitokeza kwenye mechi hiyo kwa ajili ya kuwa imara kuelekea mchezo wao unaofuata wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao utachezwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Yanga tayari imeondoka jijini Dar es salaam wakielekea mkoani Rukwa kwa kupitia Mbeya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
25m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’