Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema anafurahishwa na hali ya wachezaji wa kikosi cha Yanga hasa wale waliokuwa majeruhi ambao wameanza mazoezi.
Mkwasa amesema Yanga ilifanya uamuzi sahihi wakati wa dirisha dogo la usajili kwa kuamua kuto-ongeza wachezaji wengi wapya kwa kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi walikuwa wameanza kurejea dimbani.
Yanga imefunga usajili kwa kuongeza wachezaji wawili pekee, beki Fiston Kayembe na mshambuliaji kinda Yohana Mkomola.
TFF ilifungua dirisha dogo la usajili lililokuwa limefungwa Disemba, na sasa litafungwa Disemba 23.
Uongozi wa Yanga umesisitiza hauna mpango wala sababu ya kusajili wachezaji zaidi.
"Ukiangalia wachezaji wengi ndiyo walikuwa wanarejea kundini wakitoka kujiuguza. Sasa hauwezi kufanya usajili mkubwa badala yake kuhakikisha wanapona.
"Baada ya hapo, tutaanza kuangalia maendeleo yao, mbele huko tutajua kama tunapaswa kuongeza wachezaji au la," amefunguka Mkwasa.

ADVERTISE HERE