Luc Eymael 'awaangukia' mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2021
Luc Eymael 'awaangukia' mashabiki Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga Luc Eymael amewaomba radhi mashabiki wa Yanga na wote walioumizwa na kauli zake za kibaguzi alizotoa baada ya mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu 2019/20 dhidi ya Lipuli Fc

Eymael alitimuliwa na Yanga siku moja baada ya kutoa kauli hizo huku uongozi wa timu hiyo sambamba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakipeleka malalamiko FIFA kutokana na kauli hizo

Baadae Eymael alikata rufaa FIFA, alishinda rufaa hiyo lakini amekumbana na vikwazo vya kukosa ajira kutokana na kauli zake

Hivi karibuni alikuwa mbioni kujiunga na klabu ya Chippa United inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini, lakini mpango wa kuajiriwa na timu hiyo ulikwama baada ya Wananchi wa Afrika Kusini kupinga 'mbaguzi' wa rangi kuajiriwa nchini humo

Eymael amedai kuwa sauti yake ilieditiwa na mtu aliyefanya nae mazungumzo binafsi. Ameeleza kuwaomba radhi Wanayanga na yeyote aliyeumizwa na kauli zilizosikika

Hali imekuwa mbaya ndio anaomba radhi! Alipaswa kufanya hivi haraka baada ya 'audio' yake kuvuja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’