CV ya kocha anayetajwa kutua Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2021
CV ya kocha anayetajwa kutua Yanga

Taarifa za ujio wa kocha mpya wa Yanga Nasreddine Mohamed Nabi zilianza kuvuma tangu asubuhi ikielezwa ni suala la muda tu kocha huyo mwenye leseni ya UEFA daraja la kwanza atatua nchini na kutambulishwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga kuanzia msimu ujao

Inaelezwa kocha huyo atatua nchini akiwa na kocha msaidizi wake pamoja na Mtaalam wa viungo

Nabi ana umri wa miaka 56, amewahi kufundisha soka Libya (Al Ahly Benghazi), Sudan (Al Hilal, El Merrrikh) na hata Misri (Ismailly)

Amewahi pia kufundisha kule DR Congo klabu ya DC Motema Pembe na AC Leopards lakini pia amewahi kuwa kocha na Mkurugenzi wa Akademi ya klabu kubwa nchini Ubelgiji, RSC Anderletch

Amewahi kuwa bingwa wa ligi katika nchi tatu tofauti akiwa na AC Leopards ya Congo ( Brazaville ), DC Motema Pembe ya Congo DR na Al Hilal Omrduman ya Sudan

Kazi yake ya mwisho ilikuwa kuinoa klabu ya Al Merrikh akichukua nafasi iliyoachwa na Didier Gomes aliyetimkia Simba

Pamoja na ujio wa kocha mpya, imeelezwa kuwa Kocha Juma Mwambusi ataendelea na majukumu yake mpaka mwishoni mwa msimu

Nabi atakifanyia tathmini kikosi cha Yanga na kupendekeza maboresho ambayo atahitaji kuyafanya ili kuwa na kikosi imara msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’