Tathmini : Yanga vs Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2021
Tathmini : Yanga vs Biashara United

Ni siku nyingine kocha Juma Mwambusi atahitaji kuchanga karata zake vyema ili kuhakikisha Yanga inaondoka na alama zote tatu leo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United

Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo kule Musoma

Wananchi wanapaswa kurudia kile walichokifanya Musoma, kuweza kuwafunga Biashara Unite ambao pia katika mechi za karibuni wana 'struggle' baada ya kocha Francis Baraza kutimkia Mtibwa Sugar

Bila shaka leo Mwambusi atafanya mabadiliko katika kikosi kilichoanza mchezo uliopita dhidi ya KMC na kulazimishwa sare ya bao 1-1

Wachezaji Michael Sarpong, Carlinhos, Haruna Niyonzima, Farid Mussa na Bakari Nondo Mwamnyeto hawakuwa sehemu ya kikosi kutokana na sababu mbalimbali

Leo upo uwezekano mkubwa Mwambusi anaweza kuwatumia kutegemea na mahitaji ya mchezo

Bado safu ya ushambuliaji haijaleta matunda pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara

Kurejea kwa Carlinhos pamoja uwepo wa Saido Ntibazonkiza pengine unaweza kuleta mabadiliko katika eneo la ushambuliaji

Deus Kaseke ndiye kinara wa ufungaji kwenye kikosi cha Yanga akiwa ameweka kambani mabao sita

Huu ni mchezo ambao Mwambusi hapaswi kumuacha nje. Mikimbio ya Kaseke imekuwa na faida kubwa kwa Yanga pengine kuliko hata ile ya washambuliaji asili

Ni mchezo ambao mabadiliko makubwa ya kikosi yanatarajiwa kuonekana zaidi katika eneo la kushambulia

Beki Abdallah Shaibu Ninja alifanya vizuri katika mchezo uliopita dhidi ya KMC

Pengine Mwambusi anaweza kumuamini tena leo akianza na nahodha Lamine Moro

Mlinda lango Farouk Shikhalo anatarajiwa kuanza wakati huu ambao Metacha yuko katika majonzi ya kumpoteza mtoto wake mapema wiki hii

Kibwana Shomari na Adeyum Saleh nao huenda wakaendelea na majukumu yao kama mchezo uliopita

Hakuna shaka na nafasi za Mukoko Tonombe na Feisal Salum, kwani wamekuwa na ushirikiano mzuri katika eneo la kiungo

Katika mkutano wa Wanahabari jana kuelekea mchezo wa leo, Mwambusi alisema watacheza soka la kushambulia zaidi

Hata hivyo atapaswa kuchukua tahadhari katika ulinzi pia ili kuhakikisha yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya KMC hayajirudii

Katika mchezo huo Yanga ilikuwa ikiacha nafasi kubwa eneo la kati pale ilipokwenda kushambulia

Bryson David aliifungia KMC bao baada ya kukokota mpira kutoka umbali wa takribani mita 40 kabla ya kuachia shuti lililomshinda Shikhalo

Mwambusi anaweza kuwahitaji wachezaji aina ya Ditram Nchimbi ambao wanakuwa msaada mkubwa timu inapozuia kuanzia kwa wapinzani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’