Mashabiki wa Yanga wameaswa kuendelea kuiunga mkono timu yao kwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumamosi ijayo dhidi ya Biashara United
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku
Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC juzi, Yanga imepania kusahihisha makosa kwa kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Biashara United
Huo utakuwa mchezo wa pili kati ya michezo minne ambayo Yanga watacheza mfululizo katika uwanja wa Mkapa
Michezo mingine ni dhidi ya Gwambina Fc April 20 na Azam Fc April 25
Bado wananchi hawajakata tamaa na mbio za ubingwa hasa ikizingatiwa wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa wamekusanya alama 51
Alama nne mbele ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 47 wakati Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 46
Simba wana michezo minne ya viporo wakati Azam Fc wamecheza mechi moja zaidi ya Yanga