Tambwe atuliza mzuka Yanga, aahidi mabao ya kutosha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2017
Tambwe atuliza mzuka Yanga, aahidi mabao ya kutosha
Siku chache baada ya kurejea uwanjani, mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, amewatahadharisha mabeki wa timu pinzani kuwa amerejea na kasi kuisaidia timu yake kutetea ubingwa wake msimu huu.

Tambwe ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu, wiki hii alianza mazoezi na kucheza kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania ambapo timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana.

Akizungumza baada ya mazoezi ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Tambwe, alisema kuwa kwa sasa yupo fiti na shauku yake kubwa ni kufunga katika kila mchezo.

"Nimekaa sana nje, na nilikuwa nasononeka kukosa kucheza, kwa sasa mashabiki wasiwe na hofu, nimerejea kwa kazi moja tu, kufunga na kusaidia timu yangu kupata ushindi," alisema Tambwe.

Aidha, alisema kuwa anafahamu ushindani wa namba utakuwa mkali hasa kutokana na kuwapo kwa washambuliaji wengine kama Ibrahim Ajibu na Yohana Nkomolwa, lakini atamshawishi Kocha George Lwandamina kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Lwandamina kwa sasa ana wigo mpana wa kupanga kikosi chake kwenye safu ya ushambuliaji kufuatia kurejea kwa Tambwe na mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma, ambaye naye ameanza mazoezi wiki hii.

Kwenye michezo iliyopita ya Ligi Kuu, Lwandamina, alikuwa akiwategemea zaidi Ajibu na Obrey Chirwa kwenye safu ya ushambuliaji na wachezaji hao walionyesha uwezo na ushirikiano mkubwa.

jibu na Chirwa wamechangia kupatikana kwa mabao 17 katika michezo 11 waliyocheza huku wawili hao kwa pamoja wakiifungia Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa mabao 11
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’