Jana katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la GSM (Salamander Tower), aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Cedtic Kaze alionekana akiwa ameongozana na viongozi waandamizi wa GSM
Kaze aliachishwa majukumu yake ya kuinoa Yanga mwezi uliopita baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha
Nafasi yake ikichukuliwa na Juma Mwambusi ambaye leo ataiongoza Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Huenda Kaze akaendelea kubaki nchini taarifa za chinichini zikibainisha kuwa anaweza kupewa majukumu mengine
Akiwa kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la vijana, Kaze anaweza kufaa zaidi katika majukumu la kusimamia timu za vijana
ADVERTISE HERE