Nani aanze, nani asubiri vs KMC leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2021
Nani aanze, nani asubiri vs KMC leo?

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi leo anaanza majukumu yake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC akiwa na kikosi chake kamili

Ni Yassin Mustafa, Niyonzima, Farid Mussa na Carlinhos ambao hawatakuwa sehemu ya mchezo huo

Wananchi wanasubiri kuona kikosi ambacho Mwambusi ataanza nacho leo katika mchezo ambao Yanga inahitaji alama zote tatu

Maeneo ambayo yanaweza kuwa na mabadiliko ni katika safu ya ushambuliaji ambapo Saido Ntibazonkiza anaweza kuanza

Eneo hilo ndilo lililoonekana kuwa na changamoto zaidi lakini jana Mwambusi alisema wamefanya kazi kubwa kuboresha hivyo wananchi watarajie kuona mabadiliko

Kwenye safu ya ulinzi Adeyum Saleh anaweza kuanza kuchukua nafasi ya Yassin ambaye ni mgonjwa

Lakini pia kwa nyakati tofauti Kibwana Shomari alitumika huku kiraka Deus Kaseke akitumika kama mlinzi wa kulia kutegemeana na mfumo wa uchezaji

Mwambusi anaweza kuendelea na pacha ya walinzi wa kati manahodha Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto

Mukoko Tonombe, Feisal Salum wako vizuri kiafya wakitarajiwa kubeba majukumu ya eneo la kiungo wakati Michael Sarpong, Yacouba wanaweza kupishana eneo la ushambuliaji wakishirikiana na winga Tuisila Kisinda 'TK Master' na pengine Deus Kaseke

Eneo la mlinda lango kocha Razack Siwa atakuwa na maamuzi ya kufanya juu ya nani aanze nae katika mchezo wake wa kwanza akiwa na Metacha Mnata, Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili

Huu ni mchezo ambao benchi la ufundi linapaswa kuanza na kikosiimara ili kupata ushindi mbele ya KMC ambao imekuwa na kawaida ya 'kuivimbia' Yanga kila timu hizo zinapokutana

Msimu uliopita KMC waliondoka na alama nne dhidi ya Yanga lakini msimu huu tayari wamedondosha alama tatu mbele ya Yanga katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa jijini Mwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
44m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’