Ujio wa kocha mpya wa magolikipa Razack Siwa umemuongezea mzuka mlinda lango Ramadhani Kabwili ambaye msimu huu amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Lakini huenda Siwa akampa nafasi ligi itakaporejea wiki ijayo baada ya kumalizika kipindi cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17
Kabwili ameonekana kumvutia Siwa ambaye amefanya nae mazoezi kwa takribani wiki moja
Kwa muda mwingi msimu huu Yanga ilimtegemea zaidi mlinda lango Metacha Mnata ambaye amekuwa na msimu mzuri akiwa kinara wa 'cleansheet' (11)

Hata hivyo mwezi uliopita Metacha alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa Yanga kwa kile kilichodaiwa kuwa alichukizwa na tuhuma za hujuma alizopewa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla ambaye hata hivyo alikanusha hakumpigia simu Metacha
Ni tukio lililopelekea mashabiki wengi kupunguza imani kwake, itampasa afanye kazi ya ziada kurudisha imani hiyo
Pengine hii inaweza kuwa nafasi kwa Kabwili kupenya kwenye kikosi cha kwanza