Yanga iko katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kumleta kocha mpya kukiwa na uwezekano kwa kocha huyo kutambulishwa kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa wiki ijayo
Kumekuwa na taarifa kuwa Kocha raia wa Ufaransa Sebastian Migne huenda akatambulishwa mapema kuungana na Juma Mwambusi
Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amedokeza kuwa wanamleta kocha mpya ambaye atafanya kazi bega kwa bega na kocha Mwambusi ambaye uongozi wa Yanga umemwamini aiongoze timu mpaka mwishoni mwa msimu
Senzo amesema mpango wa Yanga kushinda ubingwa uko palepale na wanaamini ujio wa kocha mpya utaongeza ari na morali ya wachezaji kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo 11 iliyobaki
ADVERTISE HERE