Mukoko, Saido, Niyonzima kurejea Alhamisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Mar 2021
Mukoko, Saido, Niyonzima kurejea Alhamisi

Nyota watatu wa Yanga Mukoko Tomombe, Saido Ntibazonkiza na Haruna Niyonzima wanatarajia kujiunga na wenzao siku ya Alhamisi wiki hii baada ya kumaliza majukumu ya timu za Taifa

Ntibazonkiza na timu ya Taifa ya Burundi wanashuka uwanjani usiku wa leo nchini Morocco katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yanaweza kuwahakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya Afcon 2021

Niyonzima nae atakuwa dimbani nchini Cameroon kuiwakilisha Rwanda katika mchezo ambao ushindi utawapa Rwanda nafasi ya kucheza Afcon 2021

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli amesema nyota hao wanamalizia mechi leo, wameshawakatia tiketi na wataungana na wenzao Alhamisi

"Wachezaji waliokuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania''Taifa Stars'' walishawasili tangu siku ya Jumatatu, wakati Saido Ntibazonkiza(Burundi), Tomombe Mukoko(Dr Congo) na Haruna Niyonzima (Rwanda) wataanza kuwasili siku ya Alhamis"

"Yote kwa yote timu yetu inaendela vyema na mazoezi chini ya kocha Juma Mwambusi, tupo kileleni lakini pia bado tunaendelea na mchakato wa kumpata kocha mpya pindi ambapo tutakamilisha tutawatangazia.'' alisema Bumbuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’