Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama ameanza program maalum ya mazoezi ambayo itamsaidia kurejea dimbani kuendelea na majukumu yake
Ni takribani miezi 10 sasa Wananchi hawajamshuhudia fundo huyo wa mpira ambaye msimu uliopita alianza kujitengenezea ufalme ndani ya kikosi cha Yanga
Ni kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata mwishoni mwa msimu huo
Majeraha ambayo nusura yamalize maisha yake ya kusakata kabumbu. Matibabu aliyopata hapa Tanzania na baadae Afrika Kusini yamempa matumaini kuwa atarejea tena dimbani

Balama ametakiwa kuanza na program za mazoezi mepesi na kisha kufuatiwa na mazoezi magumu ambayo yatamuimarisha zaidi kabla ya kurudi uwanjani
Pengine Wananchi wanaweza kumshuhudia kabla msimu huu haujamalizika
ADVERTISE HERE