Haji Mwinyi au Gadiel Michael?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2017
Haji Mwinyi au Gadiel Michael?
Michuano ya Chalenji imemalizika jana nchini Kenya kwa Harambee Stars, wenyeji wa michuano hiyo kuibuka mabingwa baada ya kuichapa Zanzibar Heroes kwa mikwaju ya penati 3-2.

Hiyo ni baada ya sare ya mabao 2-2 katika dakika 120.

Lakini mjadala mkubwa umeibuka baina ya mashabiki wa Yanga baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha Haji Mwinyi Mngwali mlinzi wa kushoto wa Yanga na Zanzibar Heroes kwenye michuano hiyo.

Mwinyi alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Zanzibar Heroes na ndiye aliyepika bao la kwanza la kusawazisha la Zanzibar Heroes jana.

Wakati akielekea visiwani Zanzibar kujiunga na wenzake kabla ya safari ya Kenya, Mwinyi aliahidi kutumia michuano hiyo ya CECAFA Senior Challenge Cup kulishawishi benchi la Ufundi la Yanga kumpa nafasi.

Na hakika amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kiwango chake katika michuano hiyo kimetukumbusha Mwinyi Haji wa miaka miwili iliyopita.

Bila shaka benchi la ufundi limemuona, na ni swala la muda tu tutaanza kumuona tena akisaidiana na Gadiel Michael kule upande wa kushoto.

Tofauti pekee ya wawili hawa ni kwamba Mwinyi Haji ni mzuri sana katika ushambuliaji kutokea pembeni.

Krosi zake ni maridadi sana na katika michuano ya Chalenji tumemuona ameimarika sana hata katika ukabaji.

Wakati Gadiel Michael ni jembe hasa la kazi.

Faida kubwa ya Gadiel Michael ni uwezo wake wa kukaba na kushambulia bila kuchoka.

Uwepo wao wote ni faida kwa Yanga.

Bila shaka wakati huu ambao Yanga inakabiliwa na michuano mingi, mabeki hao watatumika wote.

Kwani italilazimu benchi la ufundi kubadili kikosi kwenye baadhi ya michezo ili kuwaweka wachezaji wote fiti kadiri inavyowezekana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’