Simba SC imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Libasse Gueye alianza kuifungia Simba, akimalizia pasi ya Anicet Oura, kabla ya Anthony Mligo kuongeza bao la pili. Hata hivyo, Orlando Pirates ilirejea mchezoni kupitia mabao ya Tshepang Moremi na Simphiwe Selepe, aliyemalizia pasi ya Oswin Appollis.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuanza kampeni ya Kundi C kwa pointi moja, sawa na Orlando Pirates na Colombe Sportive akishika mkia bila point, huku RS Berkane ikiongoza kundi kwa pointi tatu.
Msimamo wa Kundi C:
1. RS Berkane - Pointi 3
2. Orlando Pirates - Pointi 1
3. Simba SC - Pointi 1
4. Colombe Sportive - Pointi 0