Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Le Havre ya Ufaransa, jana alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa (Ligue 1) dhidi ya Strasbourg.
Mshambuliaji huyo alitolewa nje dakika ya 49 baada ya mwamuzi kumwadhibu kwa kosa la kucheza rafu ya hatari (serious foul play), huku Le Havre ikipoteza mchezo huo kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani.
Matokeo hayo yanaifanya Le Havre kuendelea kuwa katika wakati mgumu msimu huu, ikiwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa pointi mbili pekee baada ya michezo yake ya awali.
Hadi sasa, Le Havre haijapata ushindi wowote katika ligi, ikiwa imekusanya sare mbili pekee na kuendelea kusaka ushindi wake wa kwanza msimu huu.