Simba SC inashuka kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, saa 10:00 jioni kukabiliana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ni pambano linalokutanisha timu mbili zinazofanya vizuri katika ligi zao za ndani. Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mchezo wowote, ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa pointi 33 bila kupoteza wala kutoka sare.
Kwa upande wa Orlando Pirates, nayo imekuwa na mwendo mzuri katika ligi yake, ikiwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya vinara Mamelodi Sundowns huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Simba inaingia kwenye mtanange huo ikiwa na dhamira ya kutumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo muhimu, huku Orlando Pirates ikitaka kuonyesha ubora wake mbele ya Mnyama.
Ni vita ya wababe wawili, kila mmoja akiwa na kiu ya ushindi na dhamira ya kuanza vyema safari yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Je, Mnyama ataweza kumaliza kazi iliyowashinda wengi?