Manchester United imeendelea kupitia kipindi kigumu baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Brentford nyumbani (Old Trafford) katika mchezo wa Ligi Kuu England.
Wilson alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya United, akifunga mabao mawili dakika ya 19 na 32, kabla ya Ajer kuongeza la tatu dakika ya 82 na Schade kukamilisha ushindi huo dakika ya 91.
Kipigo hicho kinaongeza presha kwa Manchester United, ambayo sasa imeshindwa kuweka rekodi ya kutofungwa katika mechi 12 mfululizo za ligi, jambo ambalo haijawahi kutokea tangu msimu wa 1930/31.
Katika msimu huo wa 1930/31, United ilimaliza katika nafasi ya mwisho na kushuka daraja.
Pia, United imeweka rekodi isiyotamanika ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kuruhusu mabao mawili au zaidi katika kila moja ya vipindi sita mfululizo vya mechi.
Hali hiyo inaendeleza maswali kuhusu uimara wa safu ya ulinzi ya United, huku mashabiki wakisubiri kuona kama timu hiyo itaweza kurejea kwenye matokeo mazuri.