Kocha mkuu wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Abdeslam Ouaddou, amesema kikosi chake kimesafiri kuja Tanzania kikiwa na lengo la kupata ushindi dhidi ya Simba SC katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisisitiza kuwa hawana mpango wa kuridhika na sare wala kukubali kupoteza.
Ouaddou amesema mchezo huo ni muhimu katika kuanza vizuri kampeni yao ya makundi, huku akieleza kuwa wanahitaji kuzoea haraka mazingira ya Dar es Salaam ili waweze kupata matokeo wanayoyahitaji.
Kocha huyo pia amesisitiza umuhimu wa wachezaji wake kujiandaa kukabiliana na mazingira tofauti na yale wanayoyazoea nchini Afrika Kusini. Hata hivyo, hakubainisha mikakati maalumu ya kiufundi atakayotumia kuikabili Simba wala taarifa za wachezaji watakaokosekana katika mchezo huo.
Simba na Orlando Pirates zinatarajiwa kukutana apo kesho Jumapili, Novemba 29, 2026, saa 10:00 jioni, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.