Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4h ago
Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam

Tanzania imepiga hatua nyingine muhimu katika maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), kufuatia uzinduzi rasmi wa ofisi za uratibu wa mashindano hayo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameungana na Katibu Mkuu wa CAF, Samson Adamu kutoka Nigeria, pamoja na viongozi wengine kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ofisi hizo.

Hafla hiyo imefanyika leo, Jumatano, Novemba 25, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), ambapo ofisi hizo zitakuwa makao makuu ya Sekretarieti ya uratibu wa maandalizi ya AFCON 2027, iliyohamishwa kutoka Nairobi, Kenya, kwenda Dar es Salaam.

Kupitia ofisi hizo, Dar es Salaam itakuwa kiungo kikuu cha mawasiliano na uratibu kati ya CAF na nchi tatu zitakazoandaa mashindano hayo, ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Sekretarieti hiyo itahusika na uratibu wa maandalizi ya viwanja, usalama, usafiri, malazi, masuala ya kiufundi, masoko, vyombo vya habari pamoja na shughuli nyingine muhimu za mashindano hayo.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameeleza kuwa kuhamishiwa kwa ofisi hizo nchini Tanzania ni ishara ya imani ya CAF katika maandalizi yanayofanywa na nchi hiyo.

Tanzania yasema ipo tayari kwa AFCON 2027

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya AFCON 2027, Leodger Tenga, amesema Tanzania imejiandaa kwa ajili ya mashindano hayo na iko tayari kuonyesha uwezo wake katika kuandaa matukio makubwa ya kimataifa.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye.

Waziri anayesimamia michezo nchini Kenya, Salim Mvurya, pia amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki hafla hiyo.

CAF na Bodi ya Utalii Tanzania zasaini mkataba wa ushirikiano

Sambamba na uzinduzi wa ofisi hizo, CAF imesaini mkataba wa kimkakati wa ushirikiano na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), ambao unaifanya bodi hiyo kuwa mdhamini rasmi wa AFCON PAMOJA 2027.

Mkataba huo unalenga kutumia umaarufu wa soka barani Afrika na duniani kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania, kuvutia wawekezaji na kuongeza idadi ya watalii nchini.

Katibu Mkuu wa CAF, Samson Adamu, ameeleza kufurahishwa na hamasa aliyoishuhudia miongoni mwa Watanzania kuelekea mashindano hayo, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huo katika kuitangaza Tanzania kimataifa.

More Stories

BREAKING: Raheem Sterling ahukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa makosa ya barabarani
BREAKING: Raheem Sterling ahukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa makosa ya barabarani
6h ago
READ MORE β†’
Tetesi za usajili Ulaya: Liverpool, Arsenal na Man United kuwania nyota mbalimbali Januari
Tetesi za usajili Ulaya: Liverpool, Arsenal na Man United kuwania nyota mbalimbali Januari
10h ago
READ MORE β†’
Guardiola ataka Ronaldo aagwe kiheshima, asema hakustahili kumaliza safari yake kwa namna hii.
Guardiola ataka Ronaldo aagwe kiheshima, asema hakustahili kumaliza safari yake kwa namna hii.
11h ago
READ MORE β†’
UCL: Barcelona, Man United, Liverpool na Bayern Munich kazini leo
UCL: Barcelona, Man United, Liverpool na Bayern Munich kazini leo
11h ago
READ MORE β†’
Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya: Arsenal na Man City waambulia sare, Madrid wakibonda
Matokeo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya: Arsenal na Man City waambulia sare, Madrid wakibonda
20h ago
READ MORE β†’
MC Alger yaanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kukutana na Yanga
MC Alger yaanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kukutana na Yanga
21h ago
READ MORE β†’
CAS yahalalisha ubingwa wa AFCON 2025 kwa Senegal
CAS yahalalisha ubingwa wa AFCON 2025 kwa Senegal
1d ago
READ MORE β†’
Libasse afunguka siri ya ubabe wa Simba Ligi Kuu
Libasse afunguka siri ya ubabe wa Simba Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
UCL: Mechi tisa kuchezwa leo, Arsenal, Man City na Real Madrid kazini
UCL: Mechi tisa kuchezwa leo, Arsenal, Man City na Real Madrid kazini
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger
Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger
1d ago
READ MORE β†’