Kipigo cha Pyramids chaivuruga Al Ahly, yafukuza kocha, wachezaji kukatwa mishahara

Joel JJ By Joel JJ
β€’
31m ago
Kipigo cha Pyramids chaivuruga Al Ahly, yafukuza kocha, wachezaji kukatwa mishahara

Uongozi wa klabu ya Al Ahly ya Misri umefikia uamuzi wa kumfuta kazi kocha mkuu Hussein Ammouta pamoja na benchi lake la ufundi, kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Pyramids FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya viongozi wa klabu hiyo kufanya mashauriano ya dharura kutathmini mwenendo wa timu na kuweka mikakati ya kurejesha kikosi hicho katika njia ya ushindi.

Katika mchezo huo, Pyramids, inayonolewa na kocha raia wa Afrika Kusini, Rulani Mokwena, ilipata mabao yake kupitia Karim Hafez na Mostafa Fathi.

Ammouta, raia wa Morocco, anaondoka Al Ahly licha ya kuwa na rekodi nzuri tangu alipochukua jukumu la kuinoa timu hiyo mwezi Juni mwaka huu, akishinda michezo 11, kutoka sare miwili na kupoteza mchezo mmoja kati ya 14 aliyoiongoza.

Aidha, taarifa kutoka vyombo vya habari vya Misri zinaeleza kuwa uongozi wa Al Ahly umeamua kusitisha malipo ya wachezaji hadi mwenendo wa matokeo ya timu hiyo utakapoimarika.

Makamu wa Rais wa Al Ahly, Yassin Mansour, pamoja na mjumbe wa bodi ya klabu hiyo, Sayed Abdel Hafiz, wamepewa jukumu la kusimamia mchakato wa kumpata kocha mpya atakayechukua nafasi ya Ammouta.

Wakati Al Ahly ikikabiliwa na mabadiliko hayo, Mokwena anaendelea kufanya vizuri akiwa na Pyramids, ambayo imefanikiwa kushinda michezo 16 mfululizo katika mashindano yote.

Ushindi huo umeiwezesha Pyramids kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Misri ikiwa na pointi 27, ikifuatiwa na Zamalek yenye pointi 22, huku Al Ahly ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 20.

More Stories

Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger
Yanga yatangaza viingilio na mfumo wa tiketi kwa mchezo dhidi ya MC Alger
18m ago
READ MORE β†’
Mechi ya Galatasaray na Aston Villa kuwa mashakani baada ya simba kuonekana karibu na uwanja
Mechi ya Galatasaray na Aston Villa kuwa mashakani baada ya simba kuonekana karibu na uwanja
1h ago
READ MORE β†’
Al Ahly yamfuta kazi kocha wake baada ya kipigo dhidi ya Pyramids
Al Ahly yamfuta kazi kocha wake baada ya kipigo dhidi ya Pyramids
2h ago
READ MORE β†’
Kocha wa zamani Yanga aanza majukumu mapya Afrika Kusini
Kocha wa zamani Yanga aanza majukumu mapya Afrika Kusini
19h ago
READ MORE β†’
Mourinho anaamini Bernado Silva akistaafu ataiongoza Benfica
Mourinho anaamini Bernado Silva akistaafu ataiongoza Benfica
19h ago
READ MORE β†’
MC Alger watimua kocha siku chache kabla ya kukutana na Yanga CAFCL
MC Alger watimua kocha siku chache kabla ya kukutana na Yanga CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Kocha Simba ashitukia jambo, kuongeza dozi kukabiliana na ushindani
Kocha Simba ashitukia jambo, kuongeza dozi kukabiliana na ushindani
20h ago
READ MORE β†’
Hatma ya Afcon 2025 kufahamika Jumanne
Hatma ya Afcon 2025 kufahamika Jumanne
20h ago
READ MORE β†’
Pochettino aanza kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool
Pochettino aanza kwa kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool
1d ago
READ MORE β†’
Arsenal kupata pigo baada ya David Raya kuumia, vipimo zaidi kubaini hali yake
Arsenal kupata pigo baada ya David Raya kuumia, vipimo zaidi kubaini hali yake
1d ago
READ MORE β†’