Mchezo wa Galatasaray dhidi ya Aston Villa unatajwa kuwa katika hatari ya kuathiriwa baada ya taarifa za kuonekana kwa simba umbali wa takribani maili 10 kutoka uwanja utakaotumika kwa mchezo huo.
Kwa mujibu wa taarifa za Daily Mail, polisi nchini Uturuki wameanzisha msako wa kumtafuta na kumkamata mnyama huyo, huku takribani askari na maafisa 70 pamoja na ndege saba zisizo na rubani (drones) wakihusika katika zoezi hilo.
Mamlaka zinaripotiwa kubaini eneo ambalo simba huyo anasadikiwa kuwepo na zinaendelea na juhudi za kumkamata ili kuhakikisha usalama wa wakazi na watu wengine waliopo katika eneo hilo.
Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi iliyothibitisha kuahirishwa kwa mchezo huo, lakini hali hiyo imeibua wasiwasi kuhusu usalama kabla ya pambano hilo.