Arsenal imekosa nafasi ya kuweka rekodi mpya katika historia ya Ligi Kuu England baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Newcastle United katika mchezo wa ligi uliopigwa leo.
Matokeo hayo yameifanya Arsenal kushindwa kufikisha ushindi 10 katika michezo yake 11 ya mwanzo ya ligi, rekodi ambayo timu nne pekee zimewahi kuifikia na zote ziliishia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Katika mchezo huo, Arsenal ilipata mabao kupitia Eberechi Eze dakika ya 33 na Noni Madueke dakika ya 78, huku Newcastle ikifunga kupitia Harvey Barnes dakika ya 49 na Malick Thiaw dakika ya 62.
Mbali na kupoteza nafasi ya kuweka rekodi hiyo, Arsenal pia ilipata pigo baada ya kipa wake David Raya kulazimika kutoka uwanjani kutokana na jeraha. Nafasi yake ilichukuliwa na Kepa Arrizabalaga, ambaye alikuwa akicheza mchezo wake wa pili pekee wa Ligi Kuu England akiwa na Arsenal.