Arsenal yakosa kuweka rekodi ya kihistoria baada ya sare dhidi ya Newcastle

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
30m ago
Arsenal yakosa kuweka rekodi ya kihistoria baada ya sare dhidi ya Newcastle

Arsenal imekosa nafasi ya kuweka rekodi mpya katika historia ya Ligi Kuu England baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Newcastle United katika mchezo wa ligi uliopigwa leo.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal kushindwa kufikisha ushindi 10 katika michezo yake 11 ya mwanzo ya ligi, rekodi ambayo timu nne pekee zimewahi kuifikia na zote ziliishia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

Katika mchezo huo, Arsenal ilipata mabao kupitia Eberechi Eze dakika ya 33 na Noni Madueke dakika ya 78, huku Newcastle ikifunga kupitia Harvey Barnes dakika ya 49 na Malick Thiaw dakika ya 62.

Mbali na kupoteza nafasi ya kuweka rekodi hiyo, Arsenal pia ilipata pigo baada ya kipa wake David Raya kulazimika kutoka uwanjani kutokana na jeraha. Nafasi yake ilichukuliwa na Kepa Arrizabalaga, ambaye alikuwa akicheza mchezo wake wa pili pekee wa Ligi Kuu England akiwa na Arsenal.

More Stories

Prince Dube aipa Hardrock FC ubingwa Zimbabwe, afunga bao la kihistoria
Prince Dube aipa Hardrock FC ubingwa Zimbabwe, afunga bao la kihistoria
12m ago
READ MORE β†’
Simba yaendeleza ubabe Ligi Kuu, yaichapa JKT Tanzania 2-1
Simba yaendeleza ubabe Ligi Kuu, yaichapa JKT Tanzania 2-1
2h ago
READ MORE β†’
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, Ligi Kuu
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, Ligi Kuu
2h ago
READ MORE β†’
Chelsea yapokea kichapo cha aibu cha mabao 4-1 kutoka kwa Leeds United
Chelsea yapokea kichapo cha aibu cha mabao 4-1 kutoka kwa Leeds United
2h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mnyama kurejea dimbani leo, akizichapa na maafande
NBC Premier League: Mnyama kurejea dimbani leo, akizichapa na maafande
9h ago
READ MORE β†’
Super Weekend: Mechi kali za kibabe kurejea leo barani Ulaya
Super Weekend: Mechi kali za kibabe kurejea leo barani Ulaya
10h ago
READ MORE β†’
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 2-4 Singida BS, Ligi Kuu
Highlights : Azam Fc 2-4 Singida BS, Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’