Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex.
Azam ilianza vizuri kwa kupata mabao mawili ndani ya dakika mbili kupitia Feisal Salum aliyefunga kwa penalti dakika ya 28 na Zidane Sereri dakika ya 29.
Hata hivyo, Singida ilirejea mchezoni kupitia Keyekeh aliyefunga dakika ya 41, kabla ya Mwashinga kusawazisha dakika ya 51. Jonathan Sowah akawa shujaa wa Singida kwa kufunga mabao mawili dakika ya 69 na 73 na kuipa timu yake ushindi wa 4-2.
Matokeo hayo yanaifanya Singida Black Stars kuibuka kidedea katika pambano la makocha wawili kutoka DR Congo, Florent Ibenge wa Azam na Papy Kimoto wa Singida.
Ikumbukwe kuwa Azam na Singida Black Stars ni miongoni mwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CAF Confederation Cup msimu huu.
Singida imeondoka na pointi tatu muhimu, huku Azam ikipata pigo mbele ya mashabiki wake.