Ibenge apania alama tatu dhidi ya Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1d ago
Ibenge apania alama tatu dhidi ya Singida BS

Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amedhamiria kuhakikisha kikosi chake kinavuna alama zote tatu kitakaposhuka dimbani kesho Ijumaa, Novemba 20, 2026, kuikabili Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia saa 3:00 usiku, unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu hizo mbili.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Ibenge amesema anautambua ubora wa wapinzani wake, hivyo amekuwa akiyapa uzito mkubwa maandalizi ya kikosi chake ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri nyumbani.

Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema anauchukulia mchezo huo kwa uzito sawa na michezo ya hatua ya makundi ya mashindano ya kimataifa.

“Utakuwa mchezo mgumu sana. Tunauchukulia mchezo huu kwa uzito mkubwa, kama mechi ya hatua ya makundi ya michuano ya Afrika,” amesema Ibenge.

Mbali na maandalizi ya kiufundi, Ibenge amesisitiza umuhimu wa mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Azam Complex ili kuwapa nguvu wachezaji wake katika dakika zote 90 za mchezo.

“Tunahitaji sapoti yenu kubwa kesho. Mashabiki jitokezeni kwa wingi uwanjani ili muweze kuwapa nguvu wachezaji wapambane mwanzo hadi mwisho wa mchezo,” ameongeza Ibenge kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo.

Wanalambalamba hao wanarejea katika mikikimikiki ya Ligi Kuu ya NBC baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya timu za taifa, huku wakiwa na dhamira ya kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
10h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
14h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’