Soka la Argentina limekumbwa na msiba kufuatia kifo cha mchezaji chipukizi Abel Núñez, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 18 baada ya kuumia kichwani wakati wa mchezo kati ya FC Ezeiza na Deportivo Muñiz.
Núñez alianguka uwanjani baada ya kufanyiwa faulo mbaya na kugongwa kichwani na mpira. Hali yake ilihitaji msaada wa haraka wa kitabibu, huku mchezo huo ukisimamishwa kufuatia tukio hilo.
Mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura, ikiwemo kufanyiwa upasuaji, lakini baadaye alifariki dunia.
Pumzika kwa amani, Abel Núñez.