Mchezaji wa Taifa Stars na klabu ya Simba SC, Nathaniel Chilambo, ametoa ujumbe wa shukrani kwa Watanzania baada ya kupata maumivu yaliyomlazimu kushindwa kuendelea na mchezo wa apo jana dhidi ya Nigeria, huku akiahidi kurejea akiwa imara zaidi.
Kupitia ujumbe wake, Chilambo ameeleza fahari na heshima kubwa anayopata kwa kuvaa jezi ya Taifa Stars, akisisitiza kuwa kuiwakilisha Tanzania ni zaidi ya ndoto iliyotimia kwake. Amesema ni wajibu na fahari atakayoibeba maisha yake yote, huku akibainisha kuwa mapenzi ya kuitumikia nchi yake yataendelea kubaki moyoni mwake.
Mchezaji huyo amewashukuru wote waliomuunga mkono baada ya kuonekana akipata maumivu makali uwanjani na kushindwa kumaliza mchezo huo. Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi iliyowekwa wazi kuhusu aina ya jeraha lake au muda atakaohitaji kurejea uwanjani.
Chilambo alihitimisha ujumbe wake kwa maneno, βWe'll be back stronger than ever,β akimaanisha kuwa watarudi wakiwa imara zaidi kuliko wakati wowote. Kauli hiyo imeonyesha matumaini yake ya kurejea baada ya changamoto hiyo, huku mashabiki wa Simba na Taifa Stars wakisubiri taarifa zaidi kuhusu hali yake.