Chilambo avunja ukimya: 'tutarudi tukiwa imara zaidi'

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
2d ago
Chilambo avunja ukimya: 'tutarudi tukiwa imara zaidi'

Mchezaji wa Taifa Stars na klabu ya Simba SC, Nathaniel Chilambo, ametoa ujumbe wa shukrani kwa Watanzania baada ya kupata maumivu yaliyomlazimu kushindwa kuendelea na mchezo wa apo jana dhidi ya Nigeria, huku akiahidi kurejea akiwa imara zaidi.

Kupitia ujumbe wake, Chilambo ameeleza fahari na heshima kubwa anayopata kwa kuvaa jezi ya Taifa Stars, akisisitiza kuwa kuiwakilisha Tanzania ni zaidi ya ndoto iliyotimia kwake. Amesema ni wajibu na fahari atakayoibeba maisha yake yote, huku akibainisha kuwa mapenzi ya kuitumikia nchi yake yataendelea kubaki moyoni mwake.

Mchezaji huyo amewashukuru wote waliomuunga mkono baada ya kuonekana akipata maumivu makali uwanjani na kushindwa kumaliza mchezo huo. Hata hivyo, bado hakuna taarifa rasmi iliyowekwa wazi kuhusu aina ya jeraha lake au muda atakaohitaji kurejea uwanjani.

Chilambo alihitimisha ujumbe wake kwa maneno, β€œWe'll be back stronger than ever,” akimaanisha kuwa watarudi wakiwa imara zaidi kuliko wakati wowote. Kauli hiyo imeonyesha matumaini yake ya kurejea baada ya changamoto hiyo, huku mashabiki wa Simba na Taifa Stars wakisubiri taarifa zaidi kuhusu hali yake.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’