Manchester United imemteua rasmi kocha raia wa Argentina, Mauricio Pochettino, kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo baada ya kufikia makubaliano ya mwisho kuhusu mkataba wake.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Fabrizio Romano Pochettino amekubali masharti yote yaliyowasilishwa Jumatano, huku Shirikisho la Soka la Marekani (US Soccer Federation) likitoa idhini ya kukamilisha makubaliano hayo.
Ujio wa Pochettino unaashiria mwanzo wa ukurasa mpya ndani ya Manchester United, huku kocha huyo akitarajiwa kupewa jukumu la kuiongoza timu hiyo katika kipindi kijacho.