Klabu ya Manchester United imemfuta kazi kocha wake mkuu Michael Carrick kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu hiyo katika msimu huu, huku Mauricio Pochettino akitajwa kuwa chaguo kuu la kuchukua nafasi yake.
Carrick alipewa jukumu la kuinoa Manchester United mwezi Mei 2026 baada ya kufanya vizuri akiwa kocha wa muda, hatua iliyomuwezesha kupewa mkataba mpya hadi mwaka 2028. Hata hivyo, timu hiyo imeshindwa kuendeleza kiwango kilichotarajiwa, ikiwa imepata ushindi mara tatu pekee katika mashindano yote msimu huu na kushinda mchezo mmoja tu kati ya 11 iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Uingereza, uamuzi wa kumwondoa Carrick ulifikiwa baada ya tathmini iliyohusisha viongozi wa klabu, akiwemo mkurugenzi wa soka Jason Wilcox. Hali mbaya ya matokeo imeifanya United kuwa katika nafasi ya tatu kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Jina la Mauricio Pochettino limeibuka kuwa chaguo kuu la klabu hiyo. Kocha huyo wa Argentina kwa sasa anaiongoza timu ya taifa ya Marekani, na taarifa zinaeleza kuwa Manchester United imefikia makubaliano ya awali kuhusu uwezekano wa kumteua. Hata hivyo, klabu hiyo italazimika kufikia makubaliano na Shirikisho la Soka la Marekani ili kumruhusu kuondoka kwenye mkataba wake.