TFF yatangaza tarehe ya tuzo za 2025/26, tuzo mpya tatu kuongezwa

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
11 Nov 2026
TFF yatangaza tarehe ya tuzo za 2025/26, tuzo mpya tatu kuongezwa

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa hafla ya utoaji wa Tuzo za TFF kwa msimu wa 2025/26 inatarajiwa kufanyika Desemba 12, 2026, jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, tuzo hizo zitagawanywa katika makundi matano makuu ambayo ni Tuzo za Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, Ligi Nyingine pamoja na Tuzo za Utawala. Jumla ya kategoria 38 zinatarajiwa kutolewa, huku washindi 61 wakipatiwa tuzo katika maeneo mbalimbali ya soka nchini.

Katika msimu huu, TFF imeongeza kategoria mpya tatu ambazo ni Tuzo ya Mtanzania Bora Anayecheza Nje kwa upande wa wanaume, Mtanzania Bora Anayecheza Nje kwa wanawake na Kikundi Bora cha Ushangiliaji Uwanjani.

Kuongezwa kwa kategoria hizo kunalenga kupanua wigo wa kutambua mafanikio ya Watanzania wanaocheza soka nje ya nchi, sambamba na kuthamini mchango wa mashabiki katika kuhamasisha na kuunga mkono timu zao.

Hafla hiyo inatarajiwa kukutanisha wadau mbalimbali wa soka nchini kwa ajili ya kutambua na kuenzi mchango wa wachezaji, makocha, viongozi na wadau wengine waliofanya vizuri katika msimu wa 2025/26.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
5h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
10h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
11h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
14h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
19h ago
READ MORE β†’