Singida Black Stars imefafanua sababu za kufanya mabadiliko katika kikosi chake, huku ikithibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mikataba na nyota wanne kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Novemba 10, 2026, uongozi wa Singida Black Stars umesema hatua hiyo imetokana na tathmini ya kina ya kiufundi iliyofanyika baada ya kupokea maoni na maswali kutoka kwa wadau na mashabiki wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tathmini ilibaini kuwa kulikuwa na wachezaji wengi katika baadhi ya nafasi, hususan eneo la kiungo mkabaji (MD) pamoja na mawinga, hali iliyosababisha ushindani mkubwa wa namba na baadhi ya wachezaji kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Katika eneo la viungo, wachezaji waliokuwepo ni Mohamed Damaro, Lamin Sacko, Ahmed Pipino, Habib Khalidi Gego, Marcel Canadi, Sheikhan Khamis, Emmanuel Keyekeh na Dramane Kambou.
Kwa upande wa mawinga, kikosi hicho kilikuwa na Ladaki Chasambi, Henry David, Jeancy Mboma, Pomi Nzaou, Omary Omary, Nickson Mosha na Yusuph Adam.
WACHEZAJI WANNE WAFIKIA MWISHO WA SAFARI YAO SINGIDA BS
Katika hatua ya utekelezaji wa tathmini hiyo, Singida Black Stars imethibitisha kufikia makubaliano ya kuachana na wachezaji wanne kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Wachezaji hao ni:
Mohamed Damaro
Dramane Kambou
Marcel Canadi
Ladaki Chasambi
Klabu hiyo imesema makubaliano hayo yamefikiwa kwa lengo la kusitisha mikataba yao kwa njia ya amani na kwa makubaliano ya pande zote.