Manchester United inatajwa kuwa katika maandalizi ya kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, huku hatma ya kocha Michael Carrick ikiendelea kuhusishwa na uwezekano wa kuondoka klabuni hapo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, mkataba wa Carrick una kipengele kinachoruhusu kuvunjwa mapema, jambo linaloweza kupunguza gharama za klabu kumaliza mkataba wake ukilinganisha na makocha waliomtangulia.
Mauricio Pochettino anaelezwa kuwa miongoni mwa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo. Kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur na Chelsea anatajwa kuwa tayari kukubali changamoto ya kuinoa United, licha ya kuwa hivi karibuni kuongeza muda wa mkataba wake na Shirikisho la Soka la Marekani.
Majina mengine yanayojadiliwa ni Eddie Howe na Julian Nagelsmann. Hata hivyo, iwapo United itamchagua Howe, italazimika kulipa takribani pauni milioni 3 kwa Newcastle United.
Kwa sasa, macho yanaelekezwa kwa uamuzi wa mwisho wa uongozi wa Manchester United kuhusu hatma ya Carrick na kocha atakayechaguliwa kuongoza timu hiyo endapo mabadiliko yatatekelezwa.