Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappé, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba katika Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Mbappé amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo mitatu aliyocheza ndani ya mwezi huo, akifunga jumla ya mabao manne.
Mshambuliaji huyo aliendelea kuwa mhimili muhimu wa Real Madrid, akichangia matokeo mazuri ya timu hiyo katika kipindi hicho.
ADVERTISE HERE