Kocha Thomas Frank anatajwa kuwa miongoni mwa majina yanayopewa nafasi ya kuinoa Crystal Palace endapo klabu hiyo itaamua kuachana na kocha wake wa sasa, Pierre Sage.
Hadi sasa, hakuna uamuzi rasmi uliotangazwa kuhusu hatma ya Sage, lakini presha dhidi yake imeongezeka kufuatia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Liverpool siku ya Jumapili.
Matokeo hayo yameiacha Crystal Palace katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa tayari imepoteza michezo saba ya ligi msimu huu.
Kwa mujibu wa Sky Sports, Thomas Frank ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwania nafasi hiyo iwapo uongozi wa Palace utaamua kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi.
Chanzo: Sky Sports.
ADVERTISE HERE