Simba yambana Fadlu FIFA, kesi yapangiwa tarehe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18m ago
Simba yambana Fadlu FIFA, kesi yapangiwa tarehe

Sakata la kisheria kati ya klabu ya Simba SC na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fadlu Davids, linatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwezi Januari 2027.

Mzozo huo ambao umekuwa ukifuatiliwa tangu mwaka jana, unatokana na madai ya Simba dhidi ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini, ikimtuhumu kwa kuvunja masharti ya mkataba wake wakati akihudumu ndani ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa madai yaliyowasilishwa na Simba, Fadlu Davids anadaiwa kuondoka kambini mwa timu hiyo nchini Botswana bila kupata kibali maalum kutoka kwa uongozi wa klabu, kufuatia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United msimu uliopita.

Hatua hiyo ilichochea Simba kupitia Idara yake ya Sheria kuchukua hatua za kisheria kwa kuwasilisha shauri mbele ya vyombo husika vya FIFA, ikitaka kupata fidia ya kifedha kutokana na kile ilichodai kuwa ni ukiukwaji wa makubaliano ya kimkataba.

Shughuli hizo za kisheria zilisimamiwa na Idara ya Sheria ya Simba chini ya Mwanasheria wa klabu hiyo, Hosea Chamba, ambaye aliwasilisha madai hayo kwa lengo la kutetea maslahi ya klabu.

Kwa upande wa Fadlu tayari ameanza majukumu yake ya kuinoa klabu ya Yanga baada ya kutambulishwa na mabingwa hao wa kihistoria juzi.

Fadlu ametua Yanga akitoka kuhudumu klabu ya Raja CA ambayo alijiunga nayo baada ya kuondoka Simba. Aliachana na Raja CA mwishoni mwa msimu uliopita kwa makubaliano ya pande mbili.

Sasa anakiongoza kikosi cha Yanga ambacho kimeweka kambi ya maandalizi ya siku 10 visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE

More Stories

Barcelona yaichapa Atletico Madrid 2-1 ugenini, Fermin Lopez aweka rekodi nzuri
Barcelona yaichapa Atletico Madrid 2-1 ugenini, Fermin Lopez aweka rekodi nzuri
7h ago
READ MORE β†’
Manchester United na Aston Villa zagawana pointi baada ya sare ya mabao 4-4
Manchester United na Aston Villa zagawana pointi baada ya sare ya mabao 4-4
10h ago
READ MORE β†’
USM Alger yatwaa CAF Super Cup kwa kuichapa Sundowns 3-1
USM Alger yatwaa CAF Super Cup kwa kuichapa Sundowns 3-1
13h ago
READ MORE β†’
Fainali ya CAF Super Cup: Mamelodi Sundowns kukutana na USM Alger leo
Fainali ya CAF Super Cup: Mamelodi Sundowns kukutana na USM Alger leo
17h ago
READ MORE β†’
Mechi kali za leo: Atletico Madrid vs Barcelona kuwania nafasi ya kileleni La Liga
Mechi kali za leo: Atletico Madrid vs Barcelona kuwania nafasi ya kileleni La Liga
19h ago
READ MORE β†’
Messi atwaa Golden Boot ya MLS 2026, avunja rekodi ya kihistoria
Messi atwaa Golden Boot ya MLS 2026, avunja rekodi ya kihistoria
22h ago
READ MORE β†’
Nottingham Forest yaichapa Manchester City, Arsenal yaendeleza wimbi la ushindi EPL
Nottingham Forest yaichapa Manchester City, Arsenal yaendeleza wimbi la ushindi EPL
1d ago
READ MORE β†’
Yanga, Simba, Azam na Namungo wakumbana na nyundo za bodi ya Ligi (TPLB)
Yanga, Simba, Azam na Namungo wakumbana na nyundo za bodi ya Ligi (TPLB)
1d ago
READ MORE β†’
Super Weekend: Michezo minne ya EPL kuchezwa leo
Super Weekend: Michezo minne ya EPL kuchezwa leo
1d ago
READ MORE β†’
Mimi na Yanga tunalitaka taji la mabingwa Afrika: Fadlu Davids
Mimi na Yanga tunalitaka taji la mabingwa Afrika: Fadlu Davids
1d ago
READ MORE β†’